Header

Mahakama Kuu yamhukumu Lulu kwenda jela miaka 2

Mahakama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam, leo imemhukumu kifungo cha miaka miwili Elizabeth Michael Lulu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba. Hukumu imeimaliza kesi hiyo iliyodumu kwa kwa kipindi cha miaka mitano sasa.

Lulu alikuwa ameongozana na mama yake kwenye hukumu hiyo. Baada ya hukumu kutajwa, mama yake alionekana kuishiwa nguvu na kuangua kilio, huku mama yake Kanumba akilia machozi ya furaha. Tayari Lulu amepelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo chake licha ya wakili wake Kibatala kudai kuwa watakata rufaa.

Lulu alidaiwa kusabababisha kifo cha Kanumba April , 2012.

Comments

comments

You may also like ...