Header

Jaji aliyemhukumu Meek Mill kwenda jela miaka 2-4 kuchunguzwa na FBI

Jaji aliyemhukumu rapper Meek Mill kwenda jela miaka 2-4, Genece Brinkley atachunguzwa na FBI, gazeti la New York Post limeripoti. Brinkley alidaiwa kutaka afanyiwe mambo kadhaa na Meek Mill pamoja na kuonekana alikuwa akimtaka kimapenzi.

Kwa mujibu wa ripoti, Brinkley anaweza kuwa na ukaribu na meneja wa zamani wa Meek, Charlie Mack ambaye hata hivyo amekanusha kumfahamu. Wakili wa Meek, Joe Tacopina, amesema Brinkely alionesha kutofuata haki alimpohukumu Meek miaka hiyo kwa kuvunja masharti ya probation.

Tacopina alidai kuwa mwaka 2013, Brinkely alimuomba Meek aurudie wimbo wa kundi la Boyz II Men, On Bended Knee halafu amtaje kwenye wimbo huo.

Comments

comments

You may also like ...