Header

Lukaku aonyesha ubabe wake Ubelgiji akiwa na miaka 24 tu

Nyota wa Manchester United pamoja na timu ya Taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku amekuwa ndiye mfungaji bora wa muda wote katika timu ya Taifa baada ya Ushindi wa goli moja waliopata dhidi ya Japan siku ya Jana.

Lukaku, 24 amefikisha Magoli 31 katika Michezo 64 aliyochezea timu ya Taifa na kuwapiku wakongwe wa timu hiyo Bernard Voorhoof na Paul Vam Himst waliokuwa wanashikilia rekodi hiyo.

Alianza kuitumikia timu ya Taifa Mwaka 2000 akiwa na miaka 16, amefunga magoli 18 katika Mechi za kufuzu kombe la Dunia Mwaka 2018 ikiwa ni rekodi nyingine pia kwa Ubelgiji. Mpaka sasa Timu hiyo chini ya Robert Martinez haijapoteza Mchezo wowote tangu Septemba 2016 kwenye Mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania.

 

Comments

comments

You may also like ...