Header

Mama yake Irene Uwoya amlilia Ndikumana, adai alikuwa mkwe wake kipenzi

Mama yake na Irene Uwoya, ameupokea msiba wa mkwe wake Hamad Ndikumana kwa majonzi makubwa. Amesema marehemu Ndikumana alikuwa ni kama mwanae wa kuzaa na hata licha ya kuachana na binti yake, bado walikuwa wakiwasiliana sana.

Akiongea na Mtanzania Digital huku akilia kwa uchungu, Mama Irene amesema, “Hamad mimi nilimpenda, Hamad ni mtoto wa familia. Baba wa mjukuu wangu Krish, mkwe wangu nilimpenda. Dunia nzima inajua, mtoto alipendwa, hatukujali yaliyopita, hatukujali yoyote sisi tulikuwa tunafumba macho.”

Ameongeza, “Pengine alitakiwa apumzike, pengine asishuhudie machungu labda nahis kitu kama hicho, tunamuombea Mungu ampumzishe kwa amani. Sitoacha kumwombea mkwe wangu kamwe.

Ndikumana aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, amefariki usiku wa kumkia leo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.

Comments

comments

You may also like ...