Header

Mume wa zamani wa Irene Uwoya, Ndikumana aaga dunia

Aliyekuwa mume wa zamani wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, Hamad Ndikumana amefariki dunia. Ndikumana alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda.

Uongozi wa timu hiyo umesema jana mchezaji huyo wa zamani aliyejulikana pia kwa jina, Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya. Mwili wake umekutwa nyumbani kwake mjini Kigali akiwa amefariki dunia. Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajafanya ajali.

Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake.

Kwenye ndoa yake na Uwoya, Ndikumana alifanikiwa kupata mtoto wa kiume, Krish.

Comments

comments

You may also like ...