Header

Baada ya kukamata degree ya kwanza, Bill Nass aipigia hesabu Masters

Baada ya kuhitimu masomo yake, msanii wa muziki wa Hip hop nchini, Bill Nass ameonesha uwezekano wa kurudi tena darasani

Ameiambia Dizzim Online, “Mipango ya mimi kurudi darasani ipo na inawezekana kabisa upo kwasababu ukiangalia hata kozi pia niliyosomea inahitaji kujiamarisha zaidi na kutokana na kasi pia dunia inavyokwenda  sasa hivi  itafika kipindi degree itakuwa kitu cha kawaida, so lazima nijiandae kutokana na kasi na ulimwengu pia. So kuna vitu naviweka sawa nitarudi tena darasani kwa ajili ya masters.”

Akianza kusomea masters, Bill Nass atakuwa anaelekea kuungana na wasanii wengine kama Nick wa Pili na Mwana FA wenye shahada mbili.

Comments

comments

You may also like ...