Header

Linah: Sifikirii kuwa producer licha ya kumiliki studio

Linah Sanga  amesema hana mpango wa kuwa producer licha ya kuwa mmiliki wa studio yake mwenyewe ya Drop Out Entertaiment.

Ameiambia Dizzim Online, “Mimi ninachoamini kwenye fani hii kama muimbaji  basi imba kwasababu huwezi kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja, yaani kuimba na kuproduce lazima sehemu moja utaraharibu tu. Kwasababu  utajikuta mwisho wa siku  unaegemea sehemu moja, so mimi sifikirii  kuwa producer, mimi nataka kuimba  basi.”

Hivi karibuni Linah alijaaliwa kupata mtoto wa kike na bado amekuwa kimya kwenye muziki.

Comments

comments

You may also like ...