Header

‘God Father EA’ show aina ya Big Brother Brother kuanza mwakani Afrika Mashariki

Show ya TV iliyopewa jina God Father East Africa itaanza kuonekana mwakani. Reality show hiyo itahusisha nchini za Afrika Mashariki – Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda.

Usaili utaanza kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao katika majiji ya Nairobi, Kigali, Kampala na Dar es Salaam. Washiriki watakaa kwenye jumba la God Father kwa kipindi cha miezi mitatu na mshindi ataibuka na kitita cha shilingi milioni 50 za Tanzania.

Show hiyo itaonekana kupitia NTV au Citizen TV ya Kenya. Kama ilivyo Big Brother, washiriki watarekodiwa na kamera saa 24 katika siku 7.

Comments

comments

You may also like ...