Header

Daxx Cruz arusha neno la muziki kwa Diamond Platnumz, AliKiba na Tekno

Mwanamitindo maarufu kutoka nchini Tanzania anayeendesha shughuli zake za kibiashata na maisha nchini Afrika Kusini, Daxx Cruz amejibu swali la wasanii watatu bora kwake wakubwa wanaofanya vizuri katika ulimwengu wa muziki na kuwapa jukumu mashabiki la kuwapanga latika mtililiko wa jinsi watakavyo fuatana kwa ubora wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Daxx alifunguka majina matatu ya wakali wa muziki ambao aliwapa hadhi ya uwezo wao kidunia ambapo karata zake mbili za upendo zilidondokea Tanzania kwa kuwataja Diamond Platnumz, Ali Kiba na karata yake nyingine ya upendo na ya mwisho ilienda kwa mkali mwinginekutoka nchini Nigeria Tekno Miles.

Hata hivyo Mwanamitindo huyu anayefanya kazi chini ya ‘Ice Model Management’ ya Afrika Kusini ambaye pia ni mwenye kuwahi kuingiza sokoni biashara ya soksi zenye jina lake, ‘Daxx Cruz’ aliiambia Dizzim Online kuwa ni siku sio nyingi sokoni kwa mara nyingine ataweka bidhaa ya za Viatu na Sunglasses sokoni mwanzoni mwa mwa mwaka kesho(2018).

Daxx Cryz katika picha ya alipkuwa akinadi Bidhaa yake ya Soksi

 

Yasikilize mahojiano ya Dizzim Online juu ya ujio wake wa bidhaa mpya ya Viatu na miwani inayotegemewa kutoka rasmi mwanzono mwaka kesho.

 

Comments

comments

You may also like ...