Header

Nandy: Ninapenda utaratibu wa kuachia audio kabla ya video

Nandy anavutiwa zaidi na utaratibu wa kuachia audio kabla ya video. Ameiambia Dizzim Online kuwa kuanza na audio kunampa fursa ya kujua mapokezi yake.

“Hakuna tatizo lolote lile kwenye kutoa video, unajua kila mtu na mipangilio yake kwenye kazi zake mimi kama mimi napenda sana kutoa audio kwanza ili nione mashabiki wameipokeaje halafu baada ya hapo ndio nitoe video, ingawa ipo siku nitakuja kuachia vyote kwa pamoja yaani audio na video,” amesema staa huyo.

Hivi karibuni Nandy ameachia wimbo wake mpya, Kivuruge.

Comments

comments

You may also like ...