Header

Beka Flavour anza kunyemelea mdogo mdogo nyayo za Aslay

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania,Bakari Katuti a.k.a Beka Flavour ameingiza kicha chake cha muziki wake katika mfululizo wa kuachia ngoma moja baada ya ngingine ndani ya muda mithiri ya jinsi anavyoendelea kufanya Aslay.

Beka akiwa ni mkali anayebaki katika masikio ya wengi kwa ngoma ya Libebe na Sikinai, ni miezi miwili tangu amechia rasmi kazi yake aliyomshirikisha mR. Blue ‘Tuwe Sare’ kisha ‘Unanimaliza’ sasa ameachia kazi nyingine inaokwenda kwa jina ‘Sarafina’ wimbo uliofanyika Free Nation, Studio zinazomilikiwa na rapa Nay wa Mitego chini ya utayarishaji wa Awesome.

Hata hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Beka mara kwa mara amekuwa akiwatayarisha mashabiki wa muziki wake kuwa ‘Sarafina’ iko njiani hata baadhi ya picha kuonesha dalili za kuwa video ya wimbo huu wa Sarafina au Umenimaliza zinafanyika chini ya muongozaji Tonee Blaze.

Comments

comments

You may also like ...