Header

Simulizi za nyimbo za Jux zilitabiri kuachana kimapenzi na Vanessa Mdee

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Mussa a.k.a Jux imeonekana kuwa alikuwa akitoa simulizi za kimahaba katika nyimbo zake hata kusemekana kuwa upo uwezekano kuwa alitabiri kilichotokea katika mahusiano yake ya kimapenzi na Muimbaji Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee.

Kwa mujibu wa mtiririko wa kazi zake ndani ya kipindi cha miaka mitatu mpaka minne, Jux ameonekana kusimulia mtiririko wa matukio ya kimapenzi ikishabiliana na hali yake kimahusiano na Vanessa Mdee. Mwishoni mwa mwaka 2013 Jux aliachia wimbo uliokwenda kwa jina ‘Uzuri wako’ uliobeba wazo la kuusifia uzuri wa mrembo wake mwaka ambao haikuwa imethibitka kuwa tayari walishaingia katika mahusiano mazito.

Mbali na tetesi kutembe kwa kipindi huku wao wakikana kuwa katika mahusiano, Jux akiwa katika hali ya kuipromote kazi ya ‘Nikuite Nani’ mitandaoni zilianza kupita pita picha zao wakiwa pamoja katika mapozi kwa kupokezana ambayo kwa asilimia kubwa mtu ungekubali kuwa wawili hao ni zaidi ya urafiki wa kwaida kati ya mwanamke na mwanaume.

Jux na Vanessa enz wa mapenzi moto moto

Jux mashabiki wa muziki wake mwaka 2014 walikutana na kazi nyingine kwa jina ‘Nitasubiri’ wimbo ambao baadhi waliuhusisha na kipindi ambacho Jux alikuwa katika msomo nchini yake China kwa maana kuwa aliishi mbali na mpenzi wake na lilikuwa ni wazo la kusisitiza kuwa atasubiri ambapo baadae alidai kuwa wimbo huo lilikuwa ni wazo la kuwa atamsubiria Jackie Cliff kipindi ambacho alizidi kukataa kutokuwa namhusiano ya kimapenzi na Jackie.

Jux katika picha ya pamoja na wahitimu wezake nchini China

Katika kuthibitisha kuwa amezama zaidi kimapenzi kipindi ambacho taarifa rasmi zilisema kuwa anatoka kimahusiano na Vanessa, Jux mwaka 2015 aliachia kazi yake kwa jina ‘Sisikii’ kwa wazo la kuwa yuko katika dimbi la kina kirefu cha mapenzi na hasikii ambapo video ya wimbo huo ikiwa imeongozwa na Director Zed Benson na hii ndo kazi iliyozunguza kwa undani wa kuelewana na kukosana katika mapenzi ambapo waigizaji wakuu wa simulizi ya wimbo huo katika video ni Jux na Vanessa.

Katika simulizi ya wimbo huo wa Jux utagundua kuna hali ya kutolewana, kuvunjika kwa penzi kisha kusameheana na kurudiana kwa wapenzi(Jux na Vanessa) kitu ambacho mpaka sasa hakijatokea kwa wawili hao na zaidi mashabiki wanaishia kubembeleza na kutamani penzi la wawili hao kurudi ili iwe kama zamani.

Hata hivyo mabli na uchunguzi huu wa kupitia kile kinachoweza na ushabiliano wa amisha mafupi ya kimahusiano kwa Jux na Vanessa Mdee, bado wawili hao hawajaonesha dalili za kurudiana zaidi ya kuonekana katika majukwaa wakitumbuisha baadhi ya nyimbo ambazo ziliwakutanisha kwa namna moja au nyingine ukiwemo wimbo wa ‘Juu’ uliowakutanisha kwa mistari ya kujibizana kwa maneno ya kupendana na kufurahia ukaribu wao.

Comments

comments

You may also like ...