Header

Kumbukumbu ya kufariki kwa ajali ya gari kwa Sharo Millionea

Leo katika kumbukumbua ya Miaka mitano iliyopita, mashabiki wa kazi za sanaa nchini Tanzania walipokea taarifa za kumpoteza msanii, mchekeshaji na muigizaji Hussein Ramdhani a.k.a Sharo Millionare aliyefariki kwa ajali ya ya kupinduka kwa gari alilokuwa akiendesha akiwa njiani kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Lusanga Mkoani Tanga.

Kikubwa kilichowasikitisha wengi waliofikiwa na taarifa za kufariki kwa Sharo Millionare, ni umri wake mdogo katika kipindi ambacho alikuwa katika hatua za mwanzo za kupamba moto kwa umaarufu wa sanaa yake iliokuwa na aina yake ya kipekee ya uchekeshaji kitu ambacho wengi wao waliona kuwa alikuwa katika hatua za mwanzo mzuri wa kufanikiwa kwake.

Sharo Millionare alifariki akiwa ni mwenye umri wa miaka 27 na tangu kufariki kwake inahesabika kuwa kama angekuwepo angekuwa ni mwenye umri wa miaka 32 ambapo inaaminika kumbukumbu hii itarudisha sura za majonzi kwa familia, ndugu jamaa na marafiki.

Comments

comments

You may also like ...