Header

Dully Sykes: Upendo kwenye Bongo Flava umepungua

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Flava, Prince Dully Sykes, amewaomba wasanii wenzake waongeze upendo zaidi kuliko ilivyo sasa. Akipiga story na Dizzim Online, legendary huyo amesema upendo ni kitu kizuri kwakuwa kama utakuwepo uwezekano wa kusaidiana utakuwa mkubwa.

“Kiukweli upendo natamani sana uongezeke kwa sisi kama sisi wasanii ama hii tasnia kiujumla. Kwasababu ukweli ni kwamba sisi wasanii hatuna upendo kabisa, hasa kwa wale wasanii wa juu zaidi wajaribu kuleta upendo  hata kwa wale waliokuwa chini wajione na wao wapo sawa kwenye huu  mchezo,” amesema Mr Misifa.

Hivi karibuni Dully amelalamika kuwa baadhi ya wasanii wameshindwa kumpa support kwenye wimbo wake mpya Bombardier.

Comments

comments

You may also like ...