Header

Nuh Mziwanda ajipanga kuvunja ndoa, aomba kuruhusiwa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuh mziwanda ameomba ruhusa ya kuvunja ndoa katika hali ambayo baadhi ya wengi wanaofatilia muziki na maisha yake ya muziki wanazo taarifa za kuwa mkali huyu wa ‘Jike Shupa’ ndoa yake na mrembo Nawal ilivunjika miezi michache iliyopita.

Nuh na Nawal katika ndoa yao walidumu kwa muda wa takribani miezi mitano kitu ambacho zilipoanza tetesi za kuvunjika kwa ndoa yao hiyo zilikuwa kama taarifa ambazo zilizochukua muda wadau na mashabiki wa muziki wake kuamini ambapo baadae Nuh alisema kuwa mbali na kuwa wamekosana na mkewe Nawal yaani mama wa mtoto wake bado hajatoa talaka.

Kupitia ukurasa wa akaunti yake ya mtandao wa Instagram, Nuh amepost picha yake na kuweka maelezo ya kupata maoni na ruhusa kutoka kwa mashabiki wake ili aweze kuvunja ndoa ingawa haikubanika ni ndoa ipi itavunjwa na Nuh na itatumika njia ipi kutimiza hilo endapo mashabiki watatoa ruhusa ya yeye kufanya hivyo.

Najisikia kuaharibu ndoa ya Mtu'(MNANIRUHUSU AU NIKAUSHE TU 😂)watag wanao oana

A post shared by New Mziwonder 🙏 Daddy Anya 😉 (@iam_mziwanda) on

Nuh Mziwanda na Nawal walipkuwa waifunga ndoa mwaka jana

Kwa Nawal, Nuh mziwanda walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aliyepewa jina la ‘Anyagile’ na kingine kikubwa inabaki ikukumbukwa kuwa wawili hao waliweza kufunga ndoa mwezi Novemba mwaka jana inagwa sasa hivi sio wanandoa tena.

Comments

comments

You may also like ...