Header

Penzi na Jux na Vanessa Mdee laanza kuelea tena kwenye bahari ya huba

Mastaa wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na Jux baada ya panda shuka za maneno ya mashabiki huku maoni na maombi ya baadhi wakiomba warudiane kimahusiano, sasa zipo dalili za wawili hao kurudiana baada ya bembelezo zito la kimahaba katika jukwaa la tamasha la Fiesta 2017.

Kilichotokea Usiku wa tarehe 25 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es S alaam katika tamasha hilo la kihistoria Tanzania ‘Fiesta 2017’ Jux aliwatumia mastaa wakali wa sauti za kumbembeleza, Q Chillah na Kassim Mganga kaimba  nyimbo zao zilizofanya vizuri kumshawishi Vanessa atoe msamaha kwa Jux ili wawili hao warudiane.

Jukwaani dalili za wawili hao kufurahiana zilishamili hata Jux kuidondosha Microphone yake, kisha Vanessa kumbumbatia Jux kwa maneno yaliyojaa ishara ya kusameheana kwa mwendo wa kusogezana sogezana kihisia sambamba na kumbato na kiss ya midomo yao iliyochukua nafasi ya kukiweka kidoti cha penzi lao kuibuka upya.

Wachache wakaibuka kwa maoni kuwa kilichotokea ilikuwa ni moja ya njia ya kutoa burudani tu kwa mashabiki walioudhuria tamasha hilo la, kumbe haikuwa hivyo kwakuwa baadae siku iliyofuata Vanessa na Jux walineokana kupata mlo wa pamoja katika hoteli ya kifahari ya Hyatt Regency iliyoko jijini Dar Es Salaam, The Kilimanjaro kwa mujibu wa picha iliyokwekwa katika mtandao wa Instgaram na Mkurugenzi wa hoteli hiyo Nicolas Cedro.

Comments

comments

You may also like ...