Header

PSG na Man City zinavyotudhihirishia Mpira ni pesa

Katika Ligi kubwa tano Barani Ulaya kwa sasa huwezi taja ligi hizo bila kujumuisha Ligi kuu nchini England pamoja na Ligi kuu nchini Ufaransa ambazo zimekua zikifanya vizuri kwa sasa katika Michuano Mikubwa barani Ulaya ikiwemo UEFA Champions League pamoja na EUROPA Lakini pia vilabu vinavyotoka katika Ligi hizo vimekua na ushindani mkubwa ndani na hata nje ya Ligi zao.

Bila shaka tunaikumbuka Monaco ya msimu uliopita ya pale nchini Ufaransa timu ambayo ilidhihirisha kuwa kuna wakati soka si pesa pekee bali ni mbinu pamoja na ufundi wa Wachezaji pamoja na Benchi la ufundi Monaco iliishia hatua ya nusu fainali ya Michuano ya Ulaya lakini pia ilitwa Ubingwa wa Ligue 1 kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 10.

Leicester City ya msimu wa 2015-2016 ilishangaza kila mwanasoka ulimwenguni kwa kikosi cha kwaida tu ilitwaa Ubingwa wa Ligi kuu nchini England licha ya uwekezaji mdogo walioufanya kwa wachezaji wa bei rahisi lakini waliendeleza maajabu hadi katika Michuano ya UEFA ambayo waliishia hatua ya robo fainali.

Msimu huu 2017/2018 mpaka sasa Vilabu vingi vimabadili falsafa mpira kwa sasa umekua ni pesa tena pesa nyingi sana kila timu inaamini bila kufanya uwekezaji mkubwa basi haiwezi fikia malengo yake, Tuagalie kilichofanyika na Vilavu hivi viwili vyenye utajiri Mkubwa sana Manchester City na PSG.

Pep Guadiola si kocha wa kutumia pesa nyingi sana lakini imembidi katika Klabu ya Man City hatujazoea kumuona Guadiola akimaliza msimu bila kupata taji hata moja lakini msimu wake wa kwanza Man city aliondoka patupu Gudiola hakuona haja akaamua kufanya usajili wa gharama sana kavunja rekodi ya mabeki mara mbili katika dirisha moja la usajili kwa Kyle Walker pamoja na Benjamin Mendy haitoshi Guadiola akaamua kuingia sokoni kusajili Viungo pamoja na Mshambuliaji Gabriel Jesus licha ya kuwa na Wachezaji wengi na wenye uwezo kwenye kikosi.

Matokeo yake ni haya Man City mpaka sasa haijapoteza Mchezo wowote kwenye Ligi kuu nchini England Wamecheza Michezo 25 Msimu huu katika Mashindano yote na hawajapoteza na wanaongoza Ligi. Pia mpaka sasa hawajatolewa katika Mashindano yote wanayoshiriki huku wakiwa wameshatinga hatua ya 16 bora kwenye UEFA.

PSG matajiri wa Ufaransa wamekuwa na kawaida ya kutumia pesa nyingi ingawa msimu huu wametumia pesa nyingi kupitiliza, Wamevunja rekodi ya sokola usajili kwa Neymar  haitoshi wamemchukua kwa Mkopo Kyian Mbappe kutoka Monaco ambaye huenda akasajiliwa moja kwa moja na klabu hiyo kwa Pesa nyingi mwezi Januari.

Matokeo ya hayo yote hayo mpaka sasa PSG haijapoteza Mchezo wowote ikiweka rekodi ya kufunga magoli mengi katika Mashndano ya UEFA Msimu huu kwenye hatua ya makundi (magoli 24) wanaongoza Ligi kuu nchini Ufaransa na wana kila sababu ya kushinda mataji yote msimu huu kwani mpaka sasa hawajatolea katika Mshindano yote wanayoshiriki.

Kinachotokea katika Vilabu hivi maana yake ni nini? kwa sasa kila Klabu inaamini kwenye matumizi ya pesa nyingi ili kupata mafanikio ukiangalia ligi kubwa barani ulaya ni Vilabu vichache sana ambavyo vianafanya vizuri zaidi ya vilabu vilivyotumia pesa nyingi Man City na PSG ni vilabu vinavyojaribu kuaminisha mamilioni ya wapenda soka Duniani kuwa Mpira si mbinu pekee lakini ni kununua Mchezaji ambaye unahisi anafaa kwenye kikosi bila kujali gharama yake. Tusubiri Msimu huu utakapoisha tutapata Jibu kuwa pesa pekee ndiyo inatosha kuvipa Vilabu mafanikio au kuna namna nyingine.

 

Comments

comments

You may also like ...