Header

Elani ukingoni kukamilisha album baada ya kimya cha mwaka mzima

Kundi la muziki la wakali watatu kutoka nchini Kenya, ‘Elani’ linaloundwa na Wambui Ngugi, Brian Chweya na Maureen Kunga limeonekana kuwa jikoni(Studio), uwepo wao uliombatana na taarifa za kuwa kundi hilo liko katika hatua za mwisho za umaliziaji wa album yao.

Kuhusu ukamilikaji wa album ambayo bado haijatambulika kwa jina, kwa mujibu wa maneno yaliyotoka kwa mtayarishaji maarufu nchini Kenya, Patrick Mbaru ‘Saint P’ katika mtandao wa Instagram kupitia kaunti yake ameweka video iliyowaonesha wananakikundi hao wakiwa katika hali ya kupokezana mawazo ya kimuziki hata kuweka maelezo mafupi yaliyosema…”Album Almost doooooonnnneeee” ujumbe ulioashiria kuwa ni kazi iliyowachukua muda lakini sasa wako ukingoni imalizike.

Wakiwa wametimiza mwaka mmoja tangu rasmi kuachia wimbo wao wa mwisho unaokwenda kwa jina ‘Love You’ Elani hawaachia yazi yao ya pamoja kama kundi ambapo imetegemewea siku sio nyingi watatangaza ujio wao mpya.

Comments

comments

You may also like ...