Header

Linex apanga kufunga na kufungua mwaka na Mr. T Touchez

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linex Sunday Mjeda ‘Linex’ ameweka mambo sawa ya kumuwezesha kuacha kazi nyingine baada ya ‘Got Me’ na mara hii akiwa amethibitisha kuwa ujio utakaofuata umepikwa chini ya mtayarishaji Mr. T Touchez wa Touchez Sound.

Akionesha kuwa haikuwa kazi rahisi na wamefanikisha kuandaa utamu mwingine ya kazi chini ya mwavuli wa Bongo Fleva, Linex aliwaomba mashabiki kupitia ukurasa wake wa Instagram pale alipoweka picha ya Mr. T huku kuwaomba mashabiki waweke maoni na kuhaidi maoni yao endapo yatakuwa mengi kazi hiyo aliyoandaliwa na Mr. T itakuwa ni kazi ya kufunga nayo mwaka wa 2017 au vinginevyo itakuwa ni kazi ya kufungua mwaka wa 2018.

Tanx My Nigga @mrttouchez Tulichofanya Leo sio Poa kabisa comment zenu zikiwa nyingi tunafunga nalo mwaka Mapito haya litoke au tusubiri mwakani ? #VOA #MAPITO

A post shared by KABANGA HOSPITAL AMBASSADOR🇹🇿 (@linexsundaymjeda) on

Vile vile katika maelezo mafupi ya hiki cha uandaaji wa kazi akiwa na Mr. T Touchez, kwa mbali maelezo ya Linex alianza kuonekana wazi wazi kuwa wimbo huo utkwenda kwa jina ‘Mapito’ kwakuwa aliambatanisha alama ya reli yenye kitambulishi cha neno #MAPITO.

Comments

comments

You may also like ...