Header

Aslay, Dogo Richie Na Mzazi Tuva Kuwasha Moto Wa Burudani Mombasa!

 

Picha na Changez Ndzai

Aslay Kushoto, na Dogo Richie kulia

Staa wa muziki wa Bongo Flava Aslay, anatarajiwa kuangusha burudani la kukata na shoka Jumamosi hii mjini Mombasa. Mkali huyo wa vibao kama Muhudumu, Natamba, Baby na vinginevyo vingi tayari anavutia hisia za mashabiki wake kote nchini Kenya. Show hii ambayo inatarajiwa kubarikiwa na mtangazaji maarufu Africa kwasasa wakituo cha redio cha hapa nchini Kenya cha Citizen 106.7 Mzazi Willly M. Tuva na Dj nambari moja wakituo hicho hicho cha Citizen Dj Flash. Tuva ambaye umaarufu wake umepitiliza hapa Africa mashariki, ni kati ya wadau wa muziki wakizazi kipya ambao kweli wanamchango wakuinua vipaji vya mastaa wamuziki Africa mashariki wakiwemo mastaa wakubwa Africa wanaotoka kanda hii ya Africa Mashariki kupitia show yake ya burudani maarufu kama Mambo Mseto kwenye radio na MsetoEastAfrica kwenye runinga ya Citizen.

 

Hata hivyo show hii ambayo inatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa burudani wa hoteli ya kifahari maarufu kama Talentos Beach Resort. Msanii mkali na mkaazi wa mjini Mombasa Dogo Richie, anatarajiwa kuwa mwenyeji wa wageni hawa watakao toa burudani Desemba 2 2017.

 

Dogo Richie ambae anaonekana kuwazidi makali wasanii nguli wa muziki wa kizazi kipya wanao tokea kanda ya Pwani, kwakuwa kila show ya wasanii wakubwa wanaotokea Tanzania yeye huwa mwenye bahati ya kuwakaribisha na kugawanya jukwaa nao.  Ametumia ukurasa wake wa Facebook kuwajuza mashabiki wake habari hizi.Hapa nipo japo na list ndogo tu ya wasanii wakubwa wa Bongo ambao wameshawahii kulikwea jukwa moja na Dogo Richie wali. Diamond Platnumz, Ali Kiba, Shetta na wengineo. Hii inamaana thamani ya muziki na umaarufu wa Dogo Richie a.k.a Richie Ree inazidi kuapnda kila uchao. Dogo Richie kwasasa anatamba na kibao kikali kwa jina Ngojea, kibao hiki ambacho tayari kinashikilia chati za juu kwenye vituo mbalimbali za redio nchnini Kenya kimemuongezea mvuto wa mashabiki wake na pengine kikawa ndicho kimechangia yeye kuchaguliwa kulikwea jukwaa moja na Aslay Desemba 2 pale Talentos Beach Resort.

Comments

comments

You may also like ...