Header

Historia ya Miaka 15 ya Lebron nba yavunjwa na Mwamuzi

CLEVELAND, OH - NOVEMBER 01: LeBron James #23 of the Cleveland Cavaliers celebrates a second half basket while playing the Indiana Pacers at Quicken Loans Arena on November 1, 2017 in Cleveland, Ohio. Indiana won the game 124-107. NOTE TO USER: User expressly acknowledges and agrees that, by downloading and or using this photograph, User is consenting to the terms and conditions of the Getty Images License Agreement. (Photo by Gregory Shamus/Getty Images)

Kwa mara ya kwanza tangu aanze kucheza katika NBA, Nahodha wa timu ya kikapu ya Cleveland Cavaliers Lebron James ametolewa nje ya Mchezo dhidi ya Miami Heat baada ya kumtupia maneno mwamuzi wa mchezo huo.

Katika Mchezo huo ambao Cavs walishinda kwa jumla ya alama 108-97, Lebron alitolewa katika kipindi cha tatu cha Mchezo baada ya kumlalamikia Mwamuzi wa Mchezo, Kane Fitzgerald kushindwa kuamuru Faulo aliyofanyiwa Lebron dhidi ya James Johnson wa Miami ndipo mwamuzi akaamuru atolewe.

Mshindi huyo mara nne wa tuzo ya MVP alifunga jumla ya alama 21 rebound 12 huku akitoa pasi za mwisho yaani assist 6 katika Mchezo huo kabla ya kutolewa.

Mpaka Lebron anatolewa tayari cavs walikua wanaongoza kwa points 93-70 huku ikiwa imesalia dakika moja na sekunde 59 kumalizika kwa kipindi hicho cha tatu.

Comments

comments

You may also like ...