Header

Mourinho awanyamazisha wanaosema ‘anapaki Basi’

Kocha “Mbwatukaji” wa Manchester United Jose Mourinho amewaziba mdomo wanaozungumzia mfumo wake wa kujizuia kuliko kushambulia maarufu kama “kupaki basi” baada ya Klabu yake kuwa na idadi kubwa ya magoli kuliko Vilabu vingine vikubwa vinavyotumia mfumo wa kushambulia katika Ligi kuu nchini England.

Tangu msimu wa 2017/2018 wa Ligi kuu nchini England kuanza Manchester United wamefunga jumla ya magoli 32 ikiwa ni timu ya pili kufunga magoli mengi kwenye EPL, Magoli 7 zaidi ya Liverpool, 8 zaidi ya Chelsea, 9 zaidi ya Arsenal huku ikiizidi klabu ya Tottenham magoli 10.

Mourinho ameonekana kuwa na safu nzuri ya Ulinzi pamoja na Ushambuliaji, mpaka sasa timu yake imepoteza Mechi mbili tu ikiwa ni timu ya pili kupoteza Michezo michache msimu huu mbele ya Manchester City na mpaka sasa imeruhusu magoli 8 huku safu ya Ushambuliaji ikifunga jumla ya magoli 32 ambayo inaongozwa na Lukaku, Martial, Rashford pamoja na Zlatan Ibrahimovic ambaye amerejea kutoka majeruhi.

Mpaka sasa Manchester United haijapoteza Mchezo wowote katika Uwanja wa nyumbani kwenye Mashindano yote, tangu msimu uliopita hajapoteza Mechi za nyumbani ndani ya Michezo 39.

Comments

comments

You may also like ...