Header

Rihanna: Huwa nalala masaa 3 hadi 4 tu usiku

Akiwa mmoja wa waimbaji wakubwa zaidi wa muziki duniani, Rihanna kuwa na ratiba ngumu si kitu cha kushangaza. Tena, amekiri kuwa hupata shida kulala na kwamba hutumia masaa matatu hadi manne tu kuuchapa usingizi.

Mrembo huyo amefunguka kuhusu maisha yake binafsi kwenye mahojiano na jarida la Vogue Paris toleo mwezi wa 12. “I have a lot of trouble switching off. Even when I get home early, which means before 1 am, I start binge-watching shows or documentaries, which I love,’ amesema.

“I can’t go straight to bed. As a matter of fact, I only sleep three or four hours a night,” aliongeza.

Hata hivyo wataalam wanapendekeza watu wazima kuanzia miaka 18 and 60 wapaswa kulala kwa walau masaa 7 hadi 8.

Comments

comments

You may also like ...