Header

DIAMOND NA SALLAM NI DR. DRE NA JIMMY IOVINE WA AFRICA- PART.1

Diamond Kushoto Na Meneja Wake Sallam

Naanza kwa kutoa pongezi za dhati kwa mwanamuziki Diamond Platnumz, kwa jinsi maisha yake yanavyo wapa waja wengi matumaini ya kufikia malengo ya juu kimaisha. Simara moja Diamond amekuwa akiwakumbusha mashabiki wake kwamba miaka michache iliopita, alikua kijana mwenye ndoto za kuitikisa Africa na dunia kupitia muziki. Ila safari yake hiyo, hajawa rahisi licha ya kuwa mwisho wasiku amekua mafano mwema kwa wengi na jina lake kwasasa lina rindima mrindimo wa nema si hapa Africa mashariki pekee bali dunia nzima kwasasa.

Kwa upande wa pili, nataka nikuvukishe hadi nchini Marekani, ambako nguli wa muziki na muasisi wa muziki wa Hip Hop dunia kwa jina Andre Romelle Young maarufu kama Dr. Dre. Katika filamu fupi inayoelezea maisha yake na pamoja ya mwanabiashara mwenza Jimmy Iovine kwajiana ”The Difiant Ones”, kwa wale waliopata nafasi ya kuitazama utakuta msukumo wa Dr. Dre katika muziki ulitokana na mamake mazazi ambaye kunawakati alishawahi kumununulia mwanawe mashine ya mixer ilikuibua kipaji cha mwanae kama zawadi ya krisimasi. Diamond kwa upande wapili pia, mamake mzazi maekua nguzo muhimu katika kumsukuma Naseeb Abdul kufanikisha ndoto yake yakuwa staa wa muziki Africa.

Cover ya documentari ya The Dediant Ones

Hata hivyo, Dr. Dre aliaanza kupata umaarufu baada ya kuunda kundi la muziki la N.W.A lilojumulisha marraper nguli kama Ice Cube, Eazy E, MC Ren na Dj Yella mwishoni mwa miaka ya themanini. Hata hivyo kutokana na siasa na propaganda kuwa muziki wa kundi hili ulisababisha fujo mtaani, serekali ya Merikani iliiwekea vikwazo kazi za wasanii hawa nakupelekea kuvunjika kwa kundi hili. Dr. Dre alijikwamua nakusimama kidete nakusimama wima na kufungua label yake mwenye kwajina Death Row na kutoa single yake ya kwanza mwaka wa 1992 kwajina The Chronic, ambapo single hiyo iligeuka kuwa dhahabu na mwaka ulifuata wa 1993 Dr. Dre kupitia kibao hiki cha The Chronic akashida tuzo za Grammy Awards. Diamond kwa upande wake, nyuma mwaka wa 2009 baada ya kuanza kutamba. Aliwahi kukosana na producer wake wa muziki Bob Junior na kulazimika kuhamia studio nyingine, ila ikawa ndio kwanza mukoko unaalika maua. Kwani vibao alivyovifanya nje ya studio za Sharobaro records vilisababisha staa huyu kushinda tuzo zake 3 kwenye vipengele tofauti kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro mwaka 2010 nchini Tanzania.

Nikurudishe nchini Marekani, mwaka wa 1992 Dr. Dre alikutana na Jimmy Iovine ambaye pia ni muasisi wa label ya Interscope Records. Na urafiki wao wakibiashara ukazaliwa, record label hizi mbili yaani Interscope yake Jimmy Ione na Death Row ndizo zilizoleta kuzaliwa kwa marapper kama The D.O.C, Snoopy Doggy, Tupac, Eminem, Xibit, 50 Cent, The Game na sasa Fredrick Lamar. Huku Diamond Platnumz, kwa uapande wake akaja kukutana na Sallam ambaye alimutambulisha kama maneja wake. Sallam ambaye pia ni mwanabiashara, anamuchango mkubwa kwenye kuiweka kwenye ramani ya dunia nyota ya Diamond na pia kuzaliwa kwa WCB ambayo kama Dr. Dre na Jimmy Iovine pia Diamond na Sallam wakaja na mpango wakuwasaini wasaani wachanga kama Harmonize, Raymond, msanii nguli na rafikie Dimaond Rich Mavoko na Lavalava. Jumuika nami kesho tena nikiangazia kwa kina zaidi kuhusiana na uiano wa Diamond na Sallam sawia na maisha ya Dr. Dre na Jimmy Iovine…kARIB

Comments

comments

You may also like ...