Header

NEW VIDEO: ABDU KIBA X ALIKIBA- SINGLE

Ndugu wawili Alikiba na Abdu Kiba hatimae wameachilia kibao chao kipya kwajina ”Single”. Mastaa hawa wawili ambao wamebarikiwa sihaba na sauti ama vokali kali za muziki, wamekuwa wakiwaacha mashabiki wao na maswali chungu nzima kwani licha ya Alikiba kuwa na nafasi nzuri kwasasa katika muziki Africa, wameonekana kuwa mbalimbali kwa mda mrefu. Lakini hatimae, kwasasa mashabiki wakwao wanapumua kuwaona wote wawili tena wakishirikiana kwenye ngoma hii mpya kwajina Single. Ngoma ambayo kwakweli imerudisha utamu wa zama, wakati muziki wa Bongo Flava ulipokuwa unaanza kupaa. Wakati wasanii wengi wa Bongo Flava walipokuwa wakitumia locations za Tanzania haswa ufukweni mwa bahari hindi. Hebu itazame video hii hapa na utupe maoni.

Comments

comments

You may also like ...