Header

Vj Penny aeleza alivyojisikia kuimbwa na Diamond kwenye ‘Sikomi’

Mtangazaji wa TV, Penny Mungilwa aka VJ Penny, amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na kuimba kwenye wimbo mpya wa Diamond Platnumz, Sikomi. Penny ameiambia Dizzim Online kuwa hakuna kilichomshangaza.

“Kwanza nampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya  na suala la kutoa mimba ni suala ambalo muda mrefu limekuwa likizungumziwa yaani tangu zamani linaongelewa lakini kama yeye aliona sawa kulikumbushia hakuna ubaya,” amesema Penny.

Kwenye wimbo huo Diamond anasikika akisema, ‘Achana na Penny wa hidary niliyemuhongaga gari aliponambia ana mimba Mwisho wa siku akaichomoa chali.”

Comments

comments

You may also like ...