Header

DIAMOND PLATNUMZ NA SALLAM NI DR. DRE NA JIMMY IOVINE WA AFRICA -PART2

 

Makala yangu nayaendeleza, nakama jana ulikuwa unanifatilia vizuri karibu ili niweze kukujuza zaidi kwanini nasema Diamond na Sallam Sk nikama Dr. Dre na Jimmy Iovine wa Africa. Katika filamu fupi ama (Documentary) ya The Difiant Ones, Dr. Dre alikiri kuwa baada ya kuvunjika kwa kundi la muziki wa Hip Hop la N.W.A, alivunjika moyo huku akiwa ameachwa hana kitu chochote hivyo ilimubidi arudi nyumbani kwa mamake kwanza ili kuweza kujipanga upya. Hii yote ilikuwa imetokana na wimbo ambao waliimba kama kundi la N.W.A kuwatukana polisi kwa jina F**CK THE POLICE. Lakini baadaye mwaka wa 1992, alijikwamua nakuunda label yake binafsi maarufu kama Death Row. Death Row ilipigwa jeki kifedha na kampuni ya muziki ya Interscope Records inayomilikiwa mpka sasa na Jimmy Iovine. Na mwaka huohuo wa 1992, Death Row Records ikaachia kibao kipya chake Dr. Dre kwajina The Chronic. Ambacho kilipata mauzo ya hali ya juu mwaka uliofata wa 1993 na kumufanya Dr. Dre kushinda tuzo ya Grammy.

Maneja Wa Diamond Platnumz Sallam Sk a.k.a Mendez

Diamond na Sallam kwa upande mwingine baada ya kukutana, kunavitu fulani kwenye game ya muziki wa Bongo flava walivibadilisha. Sallam Sk alikuja kupiga jeki ndoto za Diamond za kuwa si bora mwanamuziki bali kuwa mwanamuziki bora. Kitu cha kwanza walichokipiga msasi ni muonekana wa Diamond (Image), wote walifahamu fika kuwa ubora wa mwanamuziki kwa wakati wote huwa ni muonekano wa nje, shukrani kwa teknolojia ya kisasa, mitandao ya kijamii ilisaidia kuitanga image ya Diamond kwa sana. Kitu cha pili ikawa ni ubora wa video, kwani tayari uimbaji wa Diamond ulikuwa unawavutia mashabiki lukuki. Hivyo waliitumia fursa hii na kuipa ubora zaidi kibiashara. Vilevile Jimmy Iovine alipokutana na Dr. Dre wakati wa mwanzoni, Dr. Dre ukumbuke alikuwa msanii wa Hip Hop tu ila biashara kwake ilikuwa bahati nasibu. Kwahivyo basi Jimmy Iovine alikuwa nakibarua cha kumunoa Dr. Dre makali nakumuweka zaidi katika hali ya ujesiriamali chambilecho Sallam Sk na Diamond.

Jimmy Iovine (Kushoto) Na Dr. Dre Kwenye Ubora Wao

Umaarufu unapotumika vizuri huleta mafao kwa mhusika, Sallam Sk alifahamu hivyo. Na alipokutana na Diamond alihakikisha kua wanatumia kila fursa kuhakikisha wanashinda kibiashara. Hadi wakati Diamond anatoa kibao Nataka kulewa mwaka wa 2012, ubora wa video wa bidhaa zake ulikuwa wa kiwango cha wastaani. Na pengine uwepo wa Sallam Sk katika label changa kwa wati huo WCB ndio uliopelekea vibao vilivyofata kama vile Kesho na My Number One kutafuta waongozaji wa video wa nchini Kenya Ogopa Djs. Na hapa ndipo sura ya ujasiriamali wa mwanamuziki Diamond Platnumz ilianza kuonekana. Kwamaana ilibidi kutumia mtonyo mrefu wa hela ili kupata ubora wa video na matunda yake yakawa ni upenyo wa muziki wa Diamond kwenye soko la Africa.

Turudi upande wa Dr. Dre na Jimmy Iovine, mwaka wa 1991, Jimmy alitambulishwa kwa lejendari wa muziki wa Hip Hop Tupac Shakhur kupitia Dr. Dre na mwaka huo akamsaini nyota huyo na mara kazi iakaanza. Ukumbuke Jimmy ndiye aliyekuwa akifadhili Record Label ya Death Row Records ya Dr. Dre pia alishughulikia matangazo ya kibiashara(Advitisements), dili za kibiashara( Endorsements) usambazaji wa nyimbo (Distribution) na kadhalika. Huku kazi kubwa ya Dr, Dre ikawa ni uzalishaji wa kazi za muziki kama mtayarishi wa muziki wa label zote mbili Interscope na Death Row. Na kama ujuavyo kilichotokea baada ya kusainiwa kwa lejendari Tupac Shakur ni historia ambayo mpaka sasa bado inaandikwa na kusomwa na mamillioni ya watu kote duniani. Diamond pia na Sallam Sk baada ya kuona mafao ya muziki yanaongezeka, walifikiria kama wanabiashara zaidi ya wasanii. Nahapo ndipo wakafungua nafasi ya kumusaini Harmonize, na tu baada ya kibao cha staa huyu kutoka wasafi kilopoachiliwa, ikawa ni kama moto uliowashwa kwenye nyasi kavu mwituni…Inaendelea!

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...