Header

Cassper Nyovest awafunika Rihanna na Justin Bieber

Cassper Nyovest ni ushahidi usemi ‘mcheza kwao hutuzwa.’ Rapper huyo Jumamosi aliweka rekodi ya kwanza nchini humo kupita show yake Fill Up FNB Stadium kwa kuuza tiketi 68,000.

Ingawa lengo lake lilikuwa ni kuuza tiketi 75,000 aliweka kuuza tiketi nyingi zaidi kuliko msanii yeyote wa Marekani au UK (kasoro U2) aliyefanya show kwenye uwanja wa FNB.

Kundi pekee ambalo limeweka rekodi kubwa ni U2 ambalo kwenye show yake ya mwaka 2011 liliuza tiketi 90,000. Rihanna aliyetumbuiza mwaka 2013 aliuza tiketi 62,000, Justin Bieber mwaka huo aliuza kopi 65,000.

Comments

comments

You may also like ...