Header

PICHA: ASLAY NA DOGO RICHY WANGUSHA BURUDANI LA MWAKA MOMBOSA!

Aslay amethibitishia wakenya kuwa kweli anauwezo wa kukidhi mahitaji yao ikizingatiwa na maswala ya burudani. Aslay ambaye weekend hii, amekuwa busy kwa ajili ya show mbili tofauti za muziki moja mjini Mombasa na yapili ilifanyika mjini Malindi katika majimbo mawili tofauti pwani mwa nchini Kenya. MC wa siku akawa ni mtangazaji maarufu barani Africa wa kituo cha redio napia televishini ya Citizen inayomilikiwa na kampuni ya habari ya Royal Media Services ya nchini Kenya.

Mombasa, Aslay alikaribishwa na staa wa muziki na anayepeperusha juu zaidi bendera ya muziki ya ukanda wa Pwani ya Kenya maarufu kama Dogo Richy. Richie Ambaye hivi sasa anatamba na kibao chake kipya kwajina Ngojea, alikwea jukwaani kwa mbwembwe kiaina huku akisindikizwa jukwaani na madancer wake. Hii inamaana yakuwa Aslay ameenza kupanda ngazi za juu kama msanii binafsi, na vibao vyake vyote wakati wote alipokuwa juu jukwaani mashabiki waliimba pamoja neno kwa lapili.

Maafisa wa usalama wakichukua piacha na Tuva

Show hii pia ilishuhudia ulinzi wa hali ya juu kutoka maafisa wa polisi wa utawala wa mjini Mombasa. Ukumbi wa Talentos ulikuwa umefurika kiasi cha haja hali ambayo ilipelekea walinzi binafsi wa wasanii hawa akiwemo Dogo Richie, Aslay na Mtangazaji Willy M. Tuva kuwa na kibarua kigumu na ndiomaana maafisa wapolisi wakaingilia kati ilikuhakikisha hali ni shwari. Lakini hata hivyo sheshe lenyewe lillikuwa la kimataifa huku Aslay akitumbuiza kwa kina na vibao vyake karibu vyote vikiwemo vile vipya. Hapa chini ni picha na taswira kamili ya hali ilivyokuwa Mombasa kwenye ukumbi wa hoteli ya kifahari ya Talentos Beach Resort.

Aslay akiporomosha burudani

Dogo Richy akifanya yake jukwaani

Madancer wa mwanamuziki Dogo Richie jukwaani

Aslay katika harakati za kuwashamoto jukwaani

Mtangazaji Willy M. Tuva na baadhi ya maafisa wa usalama

Asalya akitetemesha ukiwapagawisha mashabiki wake kwa burudani

Dogo Richie na madancer wake katika ubora wao

Aslay na Willy M. Tuva

 

Comments

comments

You may also like ...