Header

VIDEO: KALIGRAPH JONES AWAACHA WENGI MIDOMO WAZI KWA HILI!

 

Weekend hii rapper wa hapa nchini Kenya maarufu kama Kalighraph Jones, amewaacha wengi wakiwa midomo wazi. Hii nibaada ya staa huyu wa ”Unajuwa ni Mazishi”, alipoletwa jukwaani akiwa ndani ya jeneza. Jones amekua kwenye midomo ya wengi hivi majuzi, baada ya kujiingiza kwenye cheche za matusi na muigizaji na mcheshi mwenye hadhi za A list hapa nchini Kenya maarufu kama Eric Omondi. Hii nibaada ya Eric kupeperusha video iliyoonyesha kumkejeli rapper huyu.

Sasa baada ya mchepuko huo, rapper huyu ameaamua kurudi kwenye headlines tena na hili jipya, ambapo jumamosi hii, kwenye ukumbi wa Uhuru Gardens jijini Nairobi, Jones alipandishwa jukwaani akiwa kwenye ”Casket” ama jeneza la rangi nyeupe. Mashabiki na wadau wamuziki walioshuhudia hili, walishangaa kuona jeneza likiiingia jukwaani kitu kilichowafanya wote kuwa kimya kwa mda huku wakiwa na shauku kujua ninikilichokuwa kikiendelea. Lakini mwisho wa siku, mioyo iliwatua tu pale jeneza lilipofunguliwa na mara rapper huyo kutoka kwenye jeneza hilo huku akiwa ameshikilia kipaza sauti mkononi na kuanza kuimba wimbo wa unajua ni mazishi. Hebu kwa makini, tazama video hii hapa chini na toa maoni.

Comments

comments

You may also like ...