Header

DIAMOND PLATNUMZ APOKEZWA KIJITI NA FRANCO LUAMBO MAKIADI!

Diamond Platnumz Katika ubora Wake

Oktoba 12 mwaka wa 1989, muasisi wa kundi la T.P. O.K JAZZ, mpigaji gitaa, mutunzi na mwanamuziki maarufu kutoka nchi ya kidemokrasia ya Congo almaarufu kama Franco Luambo Luanzo Makiadi alivuta tama lake la mwisho la pumzi kule jijini Brussels Ubelgiji. Hii nibaada ya siku kumi pekee yani Oktoba 2 mwaka huohuo alipozaliwa msanii wa Bongo flava anayetamba kwasasa si Africa pekee bali ulimwenguni kwasasa Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz. Katika historia za mwanzoni za mastaa hawa wawili ambao maisha yao ya kuanza safari zao za muziki zina shahabiana kama shilingi kwa yapili.

Franco alianza muziki wake akiwa na umri mdogo ila alianza muziki kama kazi alipotimiza miaka kumi nasita. Franco ambaye alikuwa akiishi na mamake pekee viungani mwa mji wa Leopord Ville ambao kwasasa unajulikana kama Kinshasa, alitumia gitaa lakujitengenezea ilikuwavutia wateja kuja kununua bidhaa za mamake alizokua akiuza. Maisha haya ya chini hayakumfurahisha sana Franco na ilibidi aanze kutumbuiza watu kwenye sherehe za harusi na pia kwenye misiba ilikupata kipato zaidi. Hata hivyo aliweza kuwashawishi vijana wenzake na mwaka wa 1956 wakaunda kikundi cha muziki, ambapo walianza kucheza muziki kwenye mabaa jijini Leopord Ville(Kinshasa) na kukita kambi kwenye baa moja iliyomilikiwa na mzee mmoja kwa jina Oscar Kashama ambaye baadaye walimuenzi mzee huyo kwa kutumia herufi za jina lake za kwanza yani O.K kuunda jina la kundi lao O.K JAZZ. Japo waliliita kundi hili O.K Jazz, lakini muziki waliocheza haukua Jazz bali Rhumba iliyovutiwa sana na muziki wa Kilatino asili yake ikiwa ni nchi ya Cuba.

Diamond pia kwa upande mwingine, japokuwa babake mzazi yupo Bwana Abdul Juma ila msaada wa mamake mzazi Bi Sanura Kasimu katika msukumo mzima wakurekodi na kucheza muziki ulimfanya kufikia hatua zile amepiga kimaisha. Kwahivyo ni dhahiri shahiri kwamba mastaa wote wawili Franco Makiadi na Diamond Platnumz, mwanzoni mwa kazi zao kimuziki hawawezi kuwasahau mamazao kwa juhudi za kuwafanya mastaa wakubwa wa muziki duniani. Franco katika interviews zake nyingi alizowahi kufanyiwa miaka ya nyuma hadi kifo chake, alinukuliwa kwa mara nyingi akisema anaogopa sana kurudia nyuma katika maisha ya ufukara. Diamond pia si kwa mara moja amewahi kunukuliwa akisema kuwa kitu anachoogopa sana katika maisha yake, nikuanguka kimaisha. Ndiposa akatunga wimbo wa ”Utanipenda”, uliweza kutamba vyema. Kwenye wimbo huu Diamond alijaribu kuvuta taswira vipi hali itakavyokuwa mara tu pesa zitakavyo muishia ghafla.

Franco pia inasemakana nyimbo zake nyingi aliimba ama kutunga mambo ya mapenzi na kijamii. Diamond kwa upande mwingine nyimbo zake pia zimekua zikizunguka mapenzi na maswala ya kijamii haswa kulalama kuumizwa na wapenzi wake. Katika interview ya mwaka wa 2013, na kituo cha habari cha CCTV, bibi wa kwanza wa Franco Makiadi Bi. Pauline Mboyo alinukuliwa akisema kua Franco alitumia nyimbo kusuluhisha matatizo yakifamilia ama anapokosana na rafiki zake. ”Io unathango na biso, iokithethe somoninga ekoka ebo naye” – maana yake ”Wakati mtu alipomukosea, hakutaka kupigana naye, ila alitumia wimbo kumujibu mtu huyo na ikaishia hapo.” alinukuu Bi Pauline. Diamond pia, amekua mwepesi sana, haswa kutunga nyimbo kuwajibu wanao jaribu kumkera. Franco kupitia nyimbo kama Mario, aliweza kuwakashfu vikali watu wenye tabia kama Mario kwenye jamii ili kuacha kufanya vitendo vya aibu. Pia hivyo hivyo, Franco aliwaingilia sana wanawake kwenye tungo zake nyingi hii ni baada ya kuumizwa kimapenzi na si mara moja kitu ambacho kilimutoa imani japo hakuacha kutoka kimapenzi na wanawake lukuki katika maisha yake vivyo hivyo tunavyoshuhudia na staa Naseeb Abdul a.k.a Diamond platnumz.

Franco alipata nafasi nzuri sana kwenye serekali ya Dikteta Mobutu Seseko aliyekuwa Raisi wa nchi hiyo ya Belgium Congo ambayo kwa baadaye Mobutu aliibadilisha nakuwa Zaire. Franco alipata musukumo mkubwa kutoka kwa serekali ya Mobutu, kitu kilichomfanya kuheshimika nakuwa miongoni mwa wafrica wakwanza kuishi kwenye eneo la makazi ya wazungu jijini Kinshasa. Diamond kwa upande mwingine, amekua katika mstari wa mbele kuipeperusha bendera ya nchi yake, na hakuna mjadala hapa kwani sikwamara moja Diamond amekua akialikwa ikulu ya Raisi kwa hafla ama vitu vya kufanana na hivyo. Kitu kikubwa kilichokuwa kikimtia wasiwasi mkubwa staa Franco Luanzo Mkaiadi ni ushindani kutoka kwa Tabu Ley. Tabu Ley Rachereau, ambaye pia alikua ni mutunzi, mpigaji gita, mwanamuziki, muasisi na kiongozi wa kundi la Orchestre Afrisa International alikuwa tishio kubwa kwa Franco kwaajili ya ushindani mkuu aliyokuwa akimupa mpinzani wake. Diamond kwa upande mwingine, hali hii pia inamwia ugumu tu kwani kutoka Kariakoo King Kiba kama anavyojiita, amekua mwiba kwenye wayo wa Diamond kwa jinsi anavyompa ushindani wa hali ya juu kisa cha kuzaliwa kwa makundi mawili hasimu ya mtandaoni maarufu kama Team Kiba na Team Diamaond.

Lakini hata hivyo, kwa mktaadha huu Franco aliweza kupenya vyema nakujikimu kuwaleta wanamuziki wakali kwenye kundi lake la O.K Jazz. Ambalo ilibidi kugeuzwa jina na kuitwa Et L’Orchestre T.P.O.K Jazz mwaka wa 1974. Kundi lililoundwa na wanamuziki nguli kama Viky Longomba, Jean Serge Essous na wengine wengi huku Franco akiwa ndiye kiongozi. Lakini pia ilibidi kuwatafuta na kuwasajili wanamuziki wachanga ilikuweza kuweka kundi hili juu zaidi ya wapinzani. Hivyo mwaka wa 1975 Sam Mangwana, Simaro Litumba, 1983 pia Madilu System pia akasajiliwa na kulifanya kundi hili la muziki kuwa bora zaidi. Hata hivyo kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba katika nchi kama Ufaransa, Ubelgiji Zaire Congo DRC kulimuongezea heshima na utajiri staa huyu Franco Makiadi hivyo upendo na mapenzi aliyopewa na wengi yalipitiliza. Lakini pia, Franco Makiadi hakukosa mahadui ama wapinzani. Mwaka wa 1987 aliachilia kibao kwa jina Attetion Na SIDA(Maana Mjihadhari na Ukimwi). Mwaka huo huo miezi michache baada ya kuachilia kibao hiki, Franco alianza kuugua. Maadui wake walieneza uvumi kua Franco alikua anaugua UKIMWI. Jambo ambalo alilipinga kila wakati alipohojiwa kwenye vituo mbalimbali vya habari.

Licha ya chuki kutoka kwa upinzani, Franco aliweza kutengeneza nafasi za ajira kupitia T.P.O.K Jazz zaidi ya 44. Hii ikiwa ni lists ya wasanii wakiwemo waimbaji, wapigaji vinanda, magitaa, fundi wa mitambo, wachezaji( Dancers) na kadhalika. Diamond Platnumz pia katika team yake, licha ya kuwasajili wasanii wakiwemo waki na Harminize, Rich Mavoko, Queen Darling, Lavalava na Raymond ameweza kutengeneza nafasi za ajira nyingi zaidi na ameshawahi kunukuliwa akisema team yake iko na zaidi ya watu 20. Hii inamaana yakuwa, ukilinganisha na Franco basi wasanii hawa wanashahabiana kwa kina katika kila kitu kwenye muziki tofauti ni mda na wakati tofauti uliopo ila vingine vinabaki tu palepale. Ikiwemo pia tour za kimataifa, skendo za kila siku, uwekezaji wa mali na vinginevyo.

Comments

comments

You may also like ...