Header

Nandy adai Kivuruge ni wimbo alioununua kwa msanii chipukizi

Baadhi ya mashabiki wanadhani kuwa wimbo mpya wa Nandy, Kivuruge umebaba matukio ya kweli yaliyowahi kutokea kwenye maisha yake. Hata hivyo akizungumza na Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist (Times FM), Nandy amedai kuwa wimbo huo hakuandika yeye bali ulikuwa umesharekodiwa na msanii chipukizi wa THT na akaupenda.

“Hii nyimbo zijatunga mimi, ni nyimbo ambayo ilikuwa imeshafanywa imeingizwa sauti na mtoto wa kiume anaitwa Jay Melody pale THT. Nilivyofika nikaisikia kwa mara ya kwanza ilinichukia hisia zangu sana kwahiyo nikaona ni nyimbo kubwa. Nikamfuata Jay, nikamwambia ‘Jay I need this song niinunue sababu najua itateka watu wengi sana,” amesema Nandy.

Baada ya hapo Nandy anasema aliuvaa uhusika wa wimbo huo ndio maana watu wanahisi kuwa ameimba kile kilichowahi kumtokea.

Comments

comments

You may also like ...