Header

DIAMOND PLATNUMZ NI HABARI NYINGINE -GENIUS!

Diamond Platnumz

Diamond Platnumz kwakweli anazidi kuwashangaza na kuwakosha wengi kwa jinsi vile anvyoyabugia makopo ya maji ya mafanikio kila uchao. Hii inamfanya kuwa si staa tu bali super-staa, kwanini nasema hivi? Kunamengi sana ila kwa leo nataka nikudukulie machache tu, ambayo nahisi baada ya makala haya utakubaliana nami kuwa Diamond ni genius, na si msanii hivi hivi kutoka Tandale kama mwenyewe anvyopenda kusema. Lakini kwa bidii na ubora wamipango yake anayoifanya kila uchao inamufanya kujiweka kwenye upeo wa watu maarufu zaidi duniani.

Ngoma yake mpya Waka na Rick-Ross, ndio imechochea kabisa mimi kunukuu baadhi ya vitu vinavyomweka Diamond kuwa zaidi ya mastaa wengine, si Africa Mashariki pekee bali barani Africa kwasasa. Kitu chakwanza ambacho kimenifanya kuuandika waraka huu, ni maajabu anayoyafanya Mondi kupitia muziki. Miaka ya nyuma wengi walimucheka kwasababu kuwa hakuweza kuongea lugha ya Kimombo, ikamubidi akatafuta mwalimu ambae bila haya Diamond akafunguka kuwa ilimubidi ajifunze lugha hii ili imuezeshe kufanya biashara za kimataifa kwa urahisi. Sasa naona watu wameanza kuona mafanikio na umuhimi wa Diamond kujifunza lugha hii. Lakini pia Diamond hakujifunza tu kuandika na kuongea lugha hii, ila kuandika na kuongea kwa ufasaha hata kushinda wasomi wanaokalia vyeti vya digirii.

Kimombo kinamutihani sana haswa wakati wakuandika na kukiongea, lugha hii inachangamoto sihaba kwakweli. Mfano ni nchi ya Kenya, ambapo Kimombo ni lugha inayotumika tokea shule ya chekechea hadi chuo kikuu. Lakini asilimia hamsini ya wakenya, wanapata tabu kukiongea kimombo kwa ufasaha licha ya kuitumia lugha hii maishani mwao. Na ndio hapa Mondi anavyoingia na kuonesha kuwa yeye ni Simba kwa kila jambo analotaka kulifanya analifanya kwa ufasaha na ubora zaidi. Mpaka sasa Diamond anawashangaza wengi haswa ikizingatiwa miaka kidogo aliyotumia kujifunza kimomba, nasasa anaitumia lugha hiyo kutungia mashairi na kuongea bila shiada wala hitilafu yeyote ile.

Katika wimbo mpya na Rick Ross kwenye video hapo juu, Diamond ameitumia vyema lugha ya kimombo kana kwamba yeye alizaliwa Marekani. Mimi binafsi kama muandishi natokea Kenya, na huutumia mda mwingi sana na wasanii wakubwa hapa Kenya katika kazi yangu kama mwanahabari. Hivi unajua ni asilimia ishirini na tano pekee ya wasanii wakubwa Kenya wenye uwezo wakuandika na kuimba kwa lugha fasaha ya kimombo? Acha kuimba, unajua ni wachache kati ya wasanii wa nchini Kenya wanaoweza kuongea kimombo kwa ufasaha kwenye interviews. Pengine kwa maswali haya ndio utapata oicha kwanini namsifu Diamond kuwa hatari na tofauti na wanamuziki wengine Africa. Hali hii yakuiongea lugha ya kimombo nahata kuiimba lugha ya kiomombo, itampa fursa Diamond kueleweka kwa urahisi kwenye hatua za juu za kuutangaza zaidi muziki wake duniani. Napia biashara zake kupitia lebo yake ya WCB kumwendea vyema kimataifa, maana mawasiliano yake na wanabishara wengine duniani yanakuwa rahisi kabisa. Kwa ufupi Diamond Platnumz hajafanikiwa kimuziki pekee, ila kimaisha na inatokana na ubora wake ama kwakimombo mtu kama huyu tunamwita ”ginius”. Nahapa ndipo anapojiita Simba, huwa habahatishi tu ila yeye mwenyewe anafahamu anachokisema.

Comments

comments

You may also like ...