Header

Ni zamu ya Tekno kupewa shavu na Drake!

Drake ana mchango mkubwa kwenye mafanikio ya kimataifa ya Wizkid. Hii ni baada ya msanii huyo kushiriki kwenye remix ya wimbo Ojuelegba na kisha kumshirikisha starboy kwenye wimbo One Dance uliopo kwenye album ya mwaka 2016, Views. Kama haitoshi, Wizkid alimshirikisha tena Drizzy kwenye wimbo Come Closer.

Na sasa huenda ikawa ni zamu ya Mnaijeria mwingine kula shavu – Tekno. Rapper huyo wa Toronto amepost picha ya Tekno kwenye Insta Stories inayomuonesha akiwa amekaa nyuma ya mixer ya studio. Hajaandika kitu zaidi ya jina la Instagram la hitmaker huyo wa Pana. Baadaye Tekno amekuja kupost picha kwenye akaunti yake akiwa na Drake na kuandika: “B A S E D R O P.”

Kuna dalili kubwa ya wawili hao kusikika kwenye wimbo mmoja siku za usoni.

Comments

comments

You may also like ...