Header

Ondy G kufunga mwaka na ‘SO WILD’ f/ Nuru

Rapa kutoka nchini Kenya mwenye kofia mbili ya muziki na Udaktari, Dennis Ondigo a.k.a Ondy G amechukua maamuzi ya kuachia wimbo wake wa mwisho kwa mwaka 2017 akiwaweka tayari mashabiki kupokea kitu kingine kikubwa kitakacho muongezea heshima ya kimuziki zaidi.

Akipiga stori na Dizzim Online, Ondy G amesema kuwa ‘So Wild’ itakuwa ni kazi ya mwisho kwa mwaka 2017 na cha kutegemewa katika muziki wake ni ujio wa Album ambayo itakuwa na kazi zilizofanyika chini Tanzania na Kenya.

“Namshukuru Mwngu Mwaka sasa uko ukingoni na nikaona sio mbaya kama mashabiki nitawapo hii, Unajua mwaka huu nimejitahidi sana nisiwaangushe mashabiki wa mzuiki wangu na mwakani naamini kasi yangu haitashuka kabisa”. So Wild nimeifanya muda kidogo ulipita lakini nimeona kwa mwaka huu ni kazi ya kufunga mwaka” Amesema Ondy G.

Hata hivyo ngoma hii ni kazi iliyofanyika kwa lengo la kutoa motisha ya uwezekano wa kuyafikia mafanikio hasa ikizungumza taswira ya maisha yake binafsi ambapo Ondy G ameongeza kuwa kilichozungumzwa sio tu wazo la kisanaa bali ni hali halisi ya baadhi ya vitu vilivyotokea na vinaendelea kutokea katika maisha yake.

Itazame Video ya wimbo huo.

Comments

comments

You may also like ...