Header

Msanii wa Tip Top aliyemshirikisha Madee ajitokeza na Dkt Louis Shika

Rapa mwenye chembe kibao za kutosha za kuitwa mkali wa michano chini ya Tip Top ‘Gazza’ mwenye ujio wa kazi mpya ‘Nanii’ iliyomshirikisha Madee, ameachia video ya wimbo wake ndani ikiwa imepambwa na warembo bila kumuacha mzee mwenye sifa ya utajiri sambamba na Utata, Dkt Louis Shika.

Video ya wimbo huo iliyoongozwa na Director Khalfani, Dkt Louis Shika amepata tena nafasi ya kuonekana kwa mara nyingine ikiwa inakumbukwa kuwa tangu kupata kwake umaarufu ameonekana katika matangazo mbali mbali na video ya kazi mpya ya umoja wa masanii wawili wa muziki wa Rap, ROSTAM unoundwa na Stamina pamoja na ROMA.

Comments

comments

You may also like ...