Header

‘Nanii’ ya Gazza ft Madee yaibukiwa na waliofanya wazo la wimbo huo kabla

Gazza ni rapa aliyetambulishwa kwenye gemu la muziki wa Rap Tanzania kwa kazi mpya inayokwenda kwa jina ‘Nanii’ iliyomshirikisha Madee chini ya Tip Top na kikubwa kilchoibuka ni malalamiko ya kuingiliana na kufanana kwa wazo wa wimbo wa Nanii na wimbo mwingine uliotoka mwaka 2016 wake Cjamoker akiwashirikisha P The Mc na ZaiiD kwa jina ‘Kama Nanii’.

Kupitia ukurasa wa Instgram, P The Mc ambaye kwenye ngoma ya ‘Kama Nanii’ anasikika kwenye ubeti wa kwanza aliweka kipande kifupi cha video kinachoshabiliana kwa michano ya ZaiiD na kukiunganisha kipande hicho na kipande cha wimbo wa ‘Nanii’ kwa madai kuwa kilichofanyika ni kufanana kwa wazo la wimbo huku ikiwa wao walifanya na kuichia ngoma yao miezi kibao iliyopita.

Sikiliza nyimbo hizo kwa sikio lako nawe utupe maoni ya unachokisikia kama kweli upo ufanano wa kile kichaodaiwa hapa.

Hii  ni video wa wimbo wa Kama Nanii wake Cjamoker ft P The Mc na ZaiiD.

Huu ndo wimbo mpya wa Gazza ft. Madee – Nanii.

Comments

comments

You may also like ...