Header

Aime M ajipanga kwa jicho la kuudandia muziki wa Bongo Fleva

Aime M. baada ya kufanya vizuri na kazi yake ‘Cheza’, ameanza kujipanga na mashabulizi mapya yaliyepangwa kuoneakana mwanzoni mwa mwaka 2018 huku akisisitiza kuwa kimuziki kwa sasa ameanza kulitazama zaidi soko la Afrika Mashariki hasa nchi ya Tanzania na Bongo Fleva yake.

Akipiga stori na Dizzim Online Aime mwenye makazi yake Mjini Chicago nchini Marekani, amekiri kujifunza mengi kupitia kasi ya kukua kwa muziki wa Tanzania hata kugusia kuwa yuko katika mipango yenye dhati ya kutembelea baadhi ya miji ya Tanzania na kwa lengo la kufanya kolabo na wasanii baadhi ambao ameshawaweka katika orodha ya watakao ongeza chachu katika Album yake inayotazamiwa kuachiwa mwanzoni mwa mwaka 2018.

“Nimeona kitu kikubwa kwenye muziki wa wasanii wa East Africa na kikubwa zaidi kinaonekana kwenye huu muziki wa kuitwa Bongo Fleva ni kupanda kwa thamani ya wasanii wake wanaopata nafasi ya kuonesha vipaji vyao, So sioni sababu ya kuacha kuuchanganya muziki wangu na Bongo Fleva inayoonekana kuwa inaeleka kuwa ni bidhaa yenye kuongezeka thamani yake kila leo, Mfano mdogo ni Diamond na Ali Kiba. Hao wanapeperusha bendera ya nchi Tanzania vyema kabisa” Amesema Aime M.

Akibainisha kitakachofuata katika muziki wake mwanzoni mwa mwaka 2018, Aime M amesema kuwa anatazama mbele kukamilisha mipango yake ambayo pindi atakapo tua Tanzania atahakikisha inakamilika ili nguvu aliyopewa na mashabiki katika kutoa msaada wa kusukuma kazi yake ya Cheza ifike mbali zaidi ikiwa ni kazi yake ya kufungia mwaka huu wa 2017 pasopo kuwaangusha mashabiki wa muziki wake.

Kazi yake inayofunga mwaka 2017 kwa jina Cheza.

Comments

comments

You may also like ...