Header

J Blessing akanusha kwa nguvu kwa kinachosema juu ya ujauzito wa Avril

Muongozaji wa video za muziki na kazi mbalimbali za filamu kutoka nchini Kenya, J Blessing, amekataa ripoti zinazosambaa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa mwimbaji Avril ana mjamzito na mtoto wake.

J Blessing akikanusha kwa msimamo, alisema kuwa hana nia ya kuingia katika uhusiano na mtu mwingine kwa sasa baada ya ndoa yake kushindwa kudumu kwa mrembo aliyefanya vizuri na ngoma ya ‘Tokelezea’ Chantelle.

“Mimi niko katika mabadiliko ya maisha yangu na kila kitu kitakuwa sawa. Ambapo mimi kwa sasa nina mambo mengi sana ambayo sidhani kama uhusiano ni kitu kimoja cha kuruhusu kitawale. Kuna mengi sana katika mipango yangu, nina kazi, nina bidhaa ambazo nataka kuzitoa, nina mtoto … binti nzuri na hivyo uhusiano upo lakini uko mahali flani hivi  … “J Blessing alisema.

J Blessing alikanusha na kukataa kabisa kushiriki chochote cha kimahusiano na Avril, ambaye inaonekana kuwa ni mjamzito wa miezi minne lakini Avril mwenye  hajafunguka chochote mpaka sasa juu ya jambo hilo.

Uvumi huo wa J Blessing na Avril ulipamba moto mara tu picha ya pamoja ya wawili hao kusambaa kwa kasi mitandaoni.

 

Chanzo: SDE.

Comments

comments

You may also like ...