Header

Jimmy Chansa atokea kijeshi na kuongeza kitu kwenye jina lake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania na hitmaker wa ngoma ‘We Mchoyo’, Jimmy Chansa amedondosha video ya kazi yake mpya ‘Sijakusahau’ kazi iliyoongozwa na Director Joowzey ambapo pia imegundulika kuwa kuna kitu kimeongezeka kwenye utambulisho wake wa jina.

Mkali huyu aliyefahamika kwa kipindi kirefu kwa jina hilo la ‘Jimmy Chansa’, ameongeza neno na kuonekana kuwa kivingine sio mbaya kama utamuita ‘General Chansa’ jina ambalo limehisiwa kuibuka mara baada ya mfululizo wa picha alizoweka kupitia akaunti yake ya Instagram zilizomuonesha katika utanashati wa mavzi yenye pambo la kijeshi.

Chansa, mwanzo wa kazi hiyo, Audio imeandaliwa katika studio za AM Rec mikononi mwa watayarishaji wakali wawili, Bob Manecky na Manecky ambapo katika video Jimmy hajasita kuuvaa uhusika wa mchezo unaopendwa na asilimia kubwa ya matajiri baadhi Duniani ‘Golf’.

Hata hivyo Jimmy Chansa ameshindwa kuwaacha mashabiki wakae na kiu ya video ya wimbo huu na kuamua kuiachia mwishoni mwa mwaka 2017 kwakuwa audio ilitoka mapema mwezi Julai mwaka huu.

Comments

comments

You may also like ...