Header

Mchekeshaji Whozu alivalia njuga la picha zisizo na maadili mtandaoni

Msanii wa vichekesho na mwimbaji kutoka Tanzania Whozu ameingia kimuziki kwenye mawazo ya maadili kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram ambapo kwa upande wake wazo lake limebeba maudhui ya kiburudani yenye kukemea usambazaji wa picha zisizo na maandili.

Whozu kupitia ngoma yake mpya kwa jina ‘Follow Unfollow’ iliyofanyika chini ya prodyuza Awesome(Osam) na video ikiongozwa na Director Lucca swahili  amesikika katika uandishi wenye sababu za kumfanya amfollow mtu yeyote mwenye manufaa kwake katika mtandao huku akigusia uwekaji wa picha zisizo na maadili kuwa ni moja ya sababu zinazoweza kulazimu kukuondoa katika orodha ya watu atakaowafuata mtandaoni.

Hata hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli naye alishagusia hilo kwa upande wa sanaa ya muziki katika video na kuonesha kukerwa na uvaaji usio zingatia maadili katika video za muziki za baadhi ya wasanii kutoka Tanzania hata kutoa agizo kwa mamlaka husika(TCRA) kuvichukulia hatua kali za kisheria vituo vya matangazo endapo zitachezwa nyimbo za namna hiyo.

Comments

comments

You may also like ...