Header

TIMMY TDAT-MUZIKI UMEIPIKU NDOTO YA KUWA MCHUNGAJI WA KANISA!

Rapper wa nchini Kenya Timmy Tdat, amefungaka nakuweka wazi kuwa maisha yake ya utotoni yote alikuwa akitumikia Mungu kama mtoto wa madhabahuni kwa kimombo (Altar Boy). Akiongea na kituo kimoja cha Televisheni nchni Kenya Timothy Owor aka Timmy Tdat kama anavyofahamika na mashabiki na wadau wa muziki, amefichua kuwa babake mzazi alikuwa na ndoto yakumuona mtoto wake akiwa mchungaji wa kanisa la Katoliki. Lakini ndoto hiyo hajaweza kuwa kweli kwani Timothy Owor almaaru kama Timmy Tdat ameamua kuwa msanii wa muziki jambo ambalo anasema hajutii kabisa.

Timmy Tdat akionyesha Baadhi za Tatoo Zake kwenye Mwili Wakwake.

Mkali huyo wa ”Nimekubali” mwaka huu 2017 anafurahia kupania matunda ya kazi yake ya muziki, huku akiamini kuwa Mungu alikuwa amemupangia kazi hii kuliko ya uchungaji wa kanisa. Timmy Tdat nikati ya mastaa ambao nyimbo au kazi zao zimefanya vyema sana Africa Mashariki. Pia katika mkutadha huo, amejikuta akibugia sifa na mvuto makali wamashabiki huku collabo yake na mkali wa vokali Otile Brown kwajina ”Kasabuni” ikiwainashikilia chati mbalimbali za muziki kwenye radio na runinga zote za nchini Kenya.

 

Comments

comments

You may also like ...