Header

UHUSIANO WA WCB NA EDDY KENZO UNAZIDI KUNAWIRI!

Kupitia concert ya muziki ya mwanamuziki nguli wa nchini Uganda Eddy Kenzo iliyopewa jina”Eno Jubilation” nakudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya simu Africa Airtel Uganda, Diamond amethibitishia mashabiki wa kampuni yake ya WCB kuwa Harmonize atakwea jukwaani. Jumamosi hii ya tarehe 16 Harmonize anatarajiwa kufanya makuu kwenye ukumbi wa Jahazi pier mjini Mnyoyo nakuwakilisha WCB. Awali Eddy Kenzo alitumia ukurasa wake wa Insta kupigia mstari kuwa Harmonize atakuwa kati ya watumbuizaji watako toa burudani kwenye concert hiyo ya kufunga mwaka, huku Harmonize naye akalipigia msumari  swala hilo huku wakiachia kwikwi kwa mashabiki wa WCB na wa msanii Eddy Kenzo.

Wakati haya yanajiri mastaa hawa wawili nikimanisha Diamond Platnumz anayewakilisha Tanzania vyema duniani kupitia muziki na Eddy Kenzo anayewakilisha vyema Uganda duniani kupitia muziki pia, uhusiano wao huu kupitia muziki unaleta twasira nyingine tofauti kabisa  nzuri na yakuvutia. Diamond na Eddy Kenzo ni mfano wa kuigwa, kwani wanaonesha wazi kuwa collabo hazifanikishwi kwenye booth ya studio kwa kurekodi ngoma pekee ila hata wakati wakusaka hela kitu ambacho kinakikuza zaidi kiwanda cha muziki Africa Mashariki. Tena kwa upande mwingine mastaa hawa wawili wanawasilisha ujumbe kwa wenziwao kua bifu na figisu figisu kwenye muziki hazifaidishi ila zinabomoa muziki. Lakini pia wanamuziki wanaposhikamana pamoja nakufanya kama vile Eddy Kenzo na WCB wanavyofanya basi huenda tukashuhudia mambo mengi makubwa na pia ukuaji kupindukia kwa soko la muziki Africa.

Msanii Eddy Kenzo

Comments

comments

You may also like ...