Header

Willy Paul na ushuhuda wake wa kuvishinda vishawishi vya akina dada

Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya, Willy Paul ameweka wazo la kuvishinda vishawishi katika kazi yake mpya kwa jina ‘Tempted’ likihisiwa kuwa ni jibu la baadhi ya tuhuma za watu baadhi ya waliomsema kuwa upo uwezekano wake wa kushindwa kukabili vishawishi hasa vya wanaomfata kwa lengo la kutengeneza ukaribu unaoletelezwa na umaarufu alionao katika muziki.

Kazi hiyo iliyo fanyika chini ya usimamizi wa lebo ya muziki ya SALDIDO RECORDS na mtayarishaji Jonhtez ikiwa video imesheheni warembo na viashiria vya moto, Willy Paul amesisitiza kuwa yuko imara kushinda vishawishi hata kuwataja wakinadada wenye umaarufu mkubwa nchini Kenya, Vera Sidika na Huddah Monroe kuwa hawamyumbishi kiimani.

Willy Paul anevitaja vingi vinavyoweza kutengeneza mazingira ya mtu kujikuta katika maisha ya ushaishi wa kufanya kinachotajwa kuwa ni kwenda sambamba na dhambi na nje ya utaratibu wa maisha ya wenye nia ya kufunza kilichochema katika maisingi ya uamini wa kidini.

Comments

comments

You may also like ...