Header

Benja Musiq azungumzia uwezo wake zaidi ya kuwa Mwimbaji wa Injili

Msanii wa muziki wa Injili aliyefanya vyema na ‘Penzi lako’ kutoka Kenya, Benja Musiq amezungumzia kikubwa kingine anachoweza kufanya kama ataona uhuhimu wa kufanya hivyo katika tasnia ya muziki.

Akipiga stori na Dizizm Online, Benja amesema kuwa zaidi ya kuwa mwimbaji na muandishi wa nyimbo za Injili kama ambavyo wengi wanamjua pia ni muongozaji wa video za muziki ambaye amesharikiki katika kutengeneza na kuongoza kazi za baadhi ya wasanii nchini Kenya.

“Mimi watu wengi hawajui nina vipaji vingi katika hii muziki, mwanzoni nilianza na kupenda Kamera na nikapenda sana kushoot video za muziki na nimefanya hilo kwa some of good friends of mine na kazi zikapata kuchezwa sana hapa Kenya. Nilipoona watu waengi wanapenda kazi yangu, kitu hiyo ilinipa nzuvu na kuongeza love na mambo ya kushoot na kudirect Videos” Amesema Benja Musiq.

Benja kabla ya kuumaliza mwaka wa 2017, ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Moyoni’ iliyoongoza na Max P.I.D, audio ikiwa imekamilishwa na Prodyuza Johntez ambapo katika video ya wimbo huu amezungumzia jinsi aliepuka kuchangia chochote cha kiongozaji bali alimuachia Muongozaji Max P.I.D jukumu hilo.

“Kwenye hii kazi yangu mpya ilioongozwa na Max…sikutaka kuweka utundu na uwezo wangu wa kidirector director kwakuwa namuamini Max na ndo maana unaweza kufurahia video kwa alichokifanya” Benja Musiq Aliongeza.

Comments

comments

You may also like ...