Header

Youngkiller Msodoki aweka utundu juu ya utundu

Rapa na mkali wa Punchlines kutoka Tanzania, Youngkiller Msodoki ameachia video rasmi ya wimbo wake mpya ‘Toto tundu’ uliomshirikisha mwimbaji Bright, kazi iliyoandaliwa chini ya mikono ya Mtayarishaji Bear Beatz ‘Bear’ kutoka Studio za Kiri Rec.

Video ya wimbo huo yenye warembo waliobarikiwa na uzuri imewaka sana kwa uvaaji wa kitanashati na kupendeza sambamba na mapambo yenye ubunifu chini ya uandaaji na uongozaji wa Kwetu Studio.

Hata hivyo mkali huyu ambaye kila leo anapandisha thamani ya muziki wake na Tanznaia kwa ujumla kwa kuandaa kazi zenye ubora, amefanikisha kuwa msanii kati ya wasanii waliopata nafasi ya kushirikishwa kwenye album ya kimataifa ‘A Boy From Tandale’ yake Diamond Platnumz inayotegemewa kupatikana ikiwa kamili mtandaoni tarehe 12 mwezi Januari, 2018.

Comments

comments

You may also like ...