Header

Jason Derulo athibitisha kolabo ya Rayvanny kwenye Remix ya ‘Tip Toe’ ft. French Montana

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ ameyajwa rasmi kuwa katika kolabo ya ngoma Staa kutoka Marekani Jason Derulo baada picha iliowakilisha uwepo wa waili hao kikazi studio.

Kupitia uwanja wa maoni kwenye post ya Instagram ya Rayvanny yenye picha yao wakiwa studio, Jason Derulo alithibitisha kuwa Tip Toe Remix ndo kazi aliyoshiriki Rayvanny, ngoma ambayo awali iliwashirikisha wawili pekee, Jason Derulo na French Montana.

Kolabo hii ya wimbo wake Jason Derulo na French Montana iliyomshirikisha Rayvanny imeandika historia katika muziki wa Ukanda wa Afrika Mashariki kwa msanii kushirikishwa na Staa mkubwa wa muziki kutoka Marekani na hii inatokana na kutajwa kuwa Jason alitokea kukipenda na kukiamini kipaji cha Rayvanny kuanzia kipindi ambacho walikutana katika msimu wa Coke Studio wa mwaka 2017.

Comments

comments

You may also like ...