Header

Mr Eazi aachia video ya ‘Pour Me Water’ kutoka kwenye EP yake inayotarajiwa

 

Mkali kutoka nchini Nigeria, Mr Eazi  ameachia video ya ngoma yake “POUR ME WATER” chini ya uongozwaji wa Director ‘Teekay’  inayotegemewa kuwa kwenye orodha ya ngoma zitakazo kamilisha EP yake ijayo itakayo kwenda kwa jina “WHO IS MR EAZI?”.

Audio ya wimbo huu mpya imendaliwa na mtayarishaji wa muziki, E-Kelly ambaye ni ameshiriki kazi kibao za wakali kibao wa ukanda wa Afrika Magharibi ikiwemo ‘Leg Over’ yake Mr. Eazi iliyotoka rasmi mwishoni mwa mwaka jana.

 

Hata hivyo karibuni Mr. Eazi kabla ya kusikika kwenye hii ngoma yake mpya ‘Pour Me Water’, amesikika pia kwenye ushirikiano wa ngoma ya Mtayarishaji Otee Beatz  ‘This Year (Remix)’ ambayo pia imewashirikisha wakali wengine ambao ni pamoja na Terry G na DJ Vision.

Comments

comments

You may also like ...