Header

DOGO RICHIE- SIASA YA NCHINI KENYA IMEFUNIKA MUZIKI!

Dogo Richie

Msanii Dogo Richie ambaye kwasasa anavuma vizuri nchini Kenya kupitia muziki wake, amefunguka nakusema kuwa kipindi kizima cha uchaguzi wa nchini Kenya wasanii wamepitia wakati mgumu. Akiongea na kituo cha habari cha Swahiba 102.9 FM kilickoka kisiwani Zanzibari, Richie alimwambia mtangazaji Spesho Mtanzania kwamba zamani ama kipindi cha nyuma wakenya walikuwa wanatamba vizuri kwenye game ya muziki lakini punde tu uchaguzi ulipokaribia basi ukavuraga kabisa mitikasi yote ya muziki huku wengi wakipeana mda wao mwingi kwenye ulingo wa siasa hata kuliko muziki. Amesema licha ya Kenya kuchangia kuwasukuma wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz, AY, Jose Chameleon na wengine wengi, bado inapata changamoto za kuwatoa na kuwasupport wasanii wake kufikia viwango vya juu hali ambayo inatia wasiwasi. Kusikiliza interview yote, nimekusogezea karibu kupiti YouTube uhondo wote hapa chini. Hebu burudika.

Comments

comments

You may also like ...