Header

Romy Jones ‘RJ’ ajitumbukiza kwenye sanaa ya filamu

Dj wa Msanii Diamond Platnumz, Romy Jones ‘RJ’ amethibitisha kuwa ni wasaa mwingine wake kuonesha sura nyingine ya vipaji alivyo navyo mbali na kuwa Dj na msanii mwenye uwezo wa kuandika na muziki wa Rap.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Romy Jones ametoa taarifa ya ujio wa tamthiria aliyoshiriki inayokwenda kwa jina ‘KAPUNI’ inayotegemewa kuanza kurushwa kwenye chaneli ya Runinga ya Maisha Magic Bongo tarehe 8 Januari, 2018.

Romy aliandika kwenye post yenye picha yake…

“KAPUNI ndio itakua TAMTHILIA ama SERIES ya kwanza mimi kuonekana KUCHEZA ama KU-ACT kama moja ya ACTORS waliomo ndani…Kwemye KAPUNI Nimejaribu kuonesha kipaji changu cha upande wa pili ipasavyo…Hivyo nakuomba uwe wa kwanza kuiangalia ifikapo tarehe 8 JANUARY Ndani Ya @maishamagicbongo DSTV Channel 160…Je ungenipa character gani kwa muonekano huo????”

Romy Jons bado inabaki kuwa kijana mwenye vipaji vya haina mbali mbali kwakuwa nje ya uigizaji, kufanya za u-Dj, Rapa pia alishathibitisha kuwa na uwezo wa kuwa mtangazaji mzuri, kwa upande wa yeye kufanya muziki zipo nyimbo ambazo alizifanya hata baadhi kumshirikisha Diamond Platnumz.

Comments

comments

You may also like ...